MHE. AGGREY MWANRI ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUMKAMATA AFISA AMCOS NZEGA DC
Posted on: December 23rd, 2019
Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanry ameagiza kuwa afisa wa AMCOS Rafael Malimbi aliyekimbia akamatwe mara baada ya kutoroka na pesa za AMCOS kiasi cha shilingi Milioni kumi na tano(15M). Mkuu wa mkoa aliyaeleza hayo akiwa katika kikao cha pamoja na watendaji wa vijiji na kata na maafisa tarafa wa wilaya ya Nzega. hatuwezi kuvumilia tabia za wizi kwa watu wa jinsi hii. nilitaka nile kichwa cha afisa ushirika wa wilaya na akatoa angalizo kwa diwani ambaye ni mzazi wa mtoto kuonesha ushirikiano kwani tayari tuna saini zake na maandishi yake ili huyo kijana apatikane. Alimwagiza mkuu wa Wilaya kutaka taarifa (CV) za watu wote katika uongozi wa AMCOS katika Wilaya yake,na kama kuna yeyote aliyewahi kuonekana kuwa na sifa yoyote mbaya aondolewe katika ushirika huo. Nilazima akamatwe atiwe funzo kwa mfano wa wengine. Mmekosea njia kwa kudhani kwenye AMCOS ndiyo sehemu ya kujitajirisha umepotea, huku ni kusoma neno la Mungu. kama kuna madai ya mkulima yeyote madai yake yapelekwe kwa mkuu wa Wilaya. Juu ya kilimo cha pamba kuanzia tarehe 15/11 tuwe tumepanda zao hili. mbegu za aina mbili zote zimekubaliwa. Aliagiza kuwa kila familia itapaswa kulima hekari3, juu ya palizi mkuu wa mkoa aliwataka wakulima kutochanganya mazao maotea na mazao mapya. Aliwasisitiza watendaji kujua makadirio ya wananchi wake,ijulikane ni mbegu kiasi gani zinatakiwa na ajue mikakati ya eneo lake. Awaagiza watumishi wote ambao hawakufika katika kikao hiki wachukuliwe hatua, ikiwa kama anashindwa kufika hapa basi hata huko mtaani hutenda hivyo huo ni uzembe na hauwezi vumiliwa, hivyo alimtaka afisa utumishi na afisa kilimo kuchukua hatua mara moja. Akieleza faida ya matumizi wa mbolea na kilio kinachoendelea mpaka sasa kwa wananchi Mkuu wa Mkoa alitoa katazo kwa watumishi kwenda likizo, na kwa sababu ruhusa zimezuiliwa na ikatokea kuna yeyote a nayedai kuumwa basin a awe na uthibitisho wa maandishi na iwe kweli kama kalazwa ijulikane alomwandikia kitanda na daktari aliyemwandikia rufaa hiyo.
ili kuwa na mafanikio ya kazi ni vema kufanya kazi katika muda wa ziada, kamwe hamwezi kulingana na mikoa ya kanda ya ziwa ambayo inafanya vizuri katika kilimo cha pamba,hivyo nguvu ya ziada inatakiwa kufikia mafanikio ya wenzetu kama ilivyo kwa wanafunzi akeshaye na asiyekesha kupata A kuwa sawa ingawa nguvu wazitumiazo katika kupata hiyo A ni tofauti.
Aliwataka watumishi kuona umuhimu wa kukopa serikalini trekta. Kama unasikia serikali inakopesha halafu usikope basi una matatizo na unapaswa kwenda milembe.
Mara baada ya Mkuu wa Mkoa kuzungumza aliwataka washiriki wa semina hiyo kutoa maoni ama kuuliza maswali, Mkuu wa Polisi Wilaya aliwataka watendaji kuwaelimisha wananchi kujua umuhimu wa kutunza watoto kwani vifo vingi katika wilaya ya Nzega hutokana na madimbwi na mabwawa pia alisisitiza ulinzi hasa katika sikukuu za Krismas kwamba watendaji wahakikishe ulinzi unaimarika katika maeneo yao.
Afisa utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Ndugu Khadija Kabojela akijibu swali toka kwa mkuu wa Mkoa kuwa ana watumishi watendaji wa ngapi, alisema kuwa Halmashauri yake ina mapungufu ya watendaji 22 wa kijiji, lakini pia anashukuru serikali ya Rais Magufuli na Chama Cha Mapinduzi kwa kuleta watendaji 15 wa kata na kufanya kuwa na mapungufu ya watendaji 4 tu.
Mkuu wa mkoa amemaliza ziara yake ya siku tatu katika wilaya ya nzega iliyokuwa na uhamasishaji wa kilimo cha pamba. Upandaji miti , miti isipandwe mpaka ajiridhishe nayo kwa idadi sahihi. aliwataka watendaji kuwa na mabadiliko ya kitabia.